Zaidi ya watu bilioni 2 katika zaidi ya nchi 180 hutumia WhatsApp 1kuwasiliana na ndugu na marafiki, popote na wakati wowote. WhatsApp hailipiwi 2 na inatoa huduma rahisi, salama na ya uhakika ya kutuma ujumbe na kupiga simu, hupatikana kwenye simu kote duniani.
1 Naam, jina WhatsApp linatokana na maneno What's Up.
2 Gharama za data zinaweza kutozwa.
WhatsApp ilianza kama njia mbadala ya SMS. Bidhaa yetu sasa inasaidia kutuma na kupokea aina mbalimbali za maudhui: maandishi, picha, video, hati na eneo, pamoja na simu za sauti. Baadhi ya matukio ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikiwa kwa kutumia WhatsApp na ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwenye programu yetu. Kila uamuzi wa bidhaa unaongozwa na hamu yetu ya kuwaruhusu watu kuwasiliana popote ulimwenguni bila vizuizi.
WhatsApp ilianzishwa na Jan Koum na Brian Acton ambao hapo awali kwa pamoja walikuwa wanatumia Yahoo kwa miaka 20. WhatsApp ilijiunga na Facebook mwaka wa 2014, lakini inaendelea kufanya kazi kama programu tofauti yenye lengo maalum katika kujenga huduma ya ujumbe ambayo inafanya kazi haraka na kwa uhakika popote duniani.