Endelea kuwasiliana na Wateja wako
Unda kiungo kifupi ambacho wateja wanaweza kukitumia kuanza kupiga soga ya WhatsApp nawe. Shiriki kiungo kupitia barua pepe, tovuti yako, ukurasa wa Facebook, au njia zingine zinazotumika mara kwa mara.
Kama mwanachama wa jamii unayoitumikia, kusimamia biashara yako kunaweza kuwa vigumu zaidi kuliko kawaida wakati huu wa kutokuwa na uhakika na wakati wa utengaji. Ungana na wateja wako kwenye WhatsApp—chombo kilekile wanachotumia kuwasiliana na marafiki na familia.
Tafadhali tumia WhatsApp kwa njia nzuri unapowasiliana na wateja wako. Wasiliana tu na watumiaji unaowajua wanaotaka kupokea ujumbe kutoka kwako, waombe wateja wahifadhi nambari yako ya simu kwenye vitabu vyao vya anwani na ujiepushe na kutuma ujumbe wa kiotomatiki au matangazo ya biashara kwa vikundi. Kutofuata maadili bora ya kimsingi kunaweza kusababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine na labda kufanya akaunti kupigwa marufuku.
Ili kudhibiti vyema maswali mengi, angazia taarifa yenye manufaa katika jalada lako la biashara na ushiriki maelezo kuhusu huduma zako kwenye katalogi, tunapendekeza utumie programu ya WhatsApp Business, unayoweza kupakua bila malipo. Bofya hapa ili upate mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Programu ya WhatsApp Business. Kama unataka kuhamisha akaunti yako kutoka kwa WhatsApp Messenger kuenda kwa programu ya WhatsApp Business, bofya hapa.
Pakua kwa simu yako
Unda kiungo kifupi ambacho wateja wanaweza kukitumia kuanza kupiga soga ya WhatsApp nawe. Shiriki kiungo kupitia barua pepe, tovuti yako, ukurasa wa Facebook, au njia zingine zinazotumika mara kwa mara.
Wajulishe wateja wako kuhusu mabadiliko yoyote ya saa zako za kazi. Tumia jalada lako la biashara kuonyesha siku na saa ambazo biashara yako huwa imefunguliwa.
Julisha wateja wako kuhusu bidhaa zilizopo kwa muda halisi. Tumia vikundi katika kuwasiliana na wateja wako wakuu na usasishe katalogi yako ili wateja waone bidhaa zilizopo kwa urahisi.
Tumia video na simu za sauti zilizofumbwa katika kuwasiliana na wateja na kutoa huduma sawa na ile wamezoea kupata ana kwa ana.
Kadri matembezi na idadi ya wateja wanaokuja dukani inapopungua, huenda kukawa na ongezeka la huduma ya kuletewa bidhaa nyumbani na kujichukulia kwenye duka. Washa kipengele kinachoonyesha mahali mubashara kilicho kwenye WhatsApp, unapokaribia kufika unapopaswa kupeleka bidhaa. Kipengele hiki kinaonyesha wateja wako mahali ulipo na kinahakikisha kuwa kuna ubadilishaji wa haraka na rahisi.
Umezoea kuona wateja wakiwa wachangamfu kila wakati wanapo tembelea duka lako? Wape ziara pepe kupitia sasisho la hali.
Tumia vikundi na simu za video za vikundi kushirikiana kwa mbali.
Ukiwa na maswali yoyote yanayohusiana na Kitovu cha WhatsApp cha Habari kuhusu Virusi vya Korona, wasiliana nasi.