Jinsi WhatsApp inavyoweza kukusaidia kuendelea kuungana wakati wa janga la virusi vya korona (COVID-19)
Walimu
Ikiwa unafundisha shuleni au katika chuo kikuu, zingatia kushirikiana na wanafunzi wako kwenye WhatsApp ikiwa hali ya kawaida ya kusoma itavurugwa.*
Tafadhali tumia WhatsApp kwa njia nzuri unapowasiliana na wateja wako. Wasiliana tu na watumiaji unaowajua wanaotaka kupokea ujumbe kutoka kwako, waombe wateja wahifadhi nambari yako ya simu kwenye vitabu vyao vya anwani na ujiepushe na kutuma ujumbe wa kiotomatiki au matangazo ya biashara kwa vikundi. Kutofuata maadili bora ya kimsingi kunaweza kusababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine na labda kufanya akaunti kupigwa marufuku.
Ikiwa hujawahi kutumia WhatsApp, bofya hapa ili upate mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuanza kutumia WhatsApp.
Endelea kuwasiliana na wanafunzi wako
Ikiwa bado huna nambari za simu za wanafunzi, unda kiungo jumuishi ambacho wanafunzi wanaweza kutumia kuanzisha soga ya WhatsApp nawe. Shiriki kiungo kupitia barua pepe, ukurasa wako wa Facebook, au njia nyingine zisizo za umma.
Tumia WhatsApp kuwasilisha mafunzo
Shiriki mafunzo kwa njia ya maandishi na ujumbe wa sauti. Simamia majadiliano kati ya wanafunzi, jinsi tu unavyofanya ukiwa nao moja kwa moja, kwa kuunda kikundi cha kila darasa.
Tuma na upokee kazi
Tumia orodha za matangazo kuwapatia wanafunzi wengi kazi ya ziada, kwa wakati mmoja. Ni watu unaowasiliana nao pekee, ambao wamekuongeza kwenye vitabu vyao vya anwani watapokea ujumbe wa tangazo lako. Majibu yatakwenda kwako tu ili wanafunzi waweze kujibu na kazi zilizokamilika.
Tuma ujumbe kutoka kwenye kompyuta yako
Tumia WhatsApp Web kudhibiti idadi kubwa ya ujumbe wa WhatsApp kwa njia ya haraka na rahisi kwa kutumia kompyuta yako ya dawati.
*WhatsApp inaruhusiwa tu kutumika kulingana na sheria husika na Sheria na Masharti ya WhatsApp, ikiwa ni pamoja na umri wa chini sana unaoruhusiwa kutumia huduma zetu. Usiwahimize wanafunzi au watu wengine watumie WhatsApp ikiwa bado hawajatimiza umri unaoruhusiwa, au kuwalazimisha wanafunzi kutumia WhatsApp
Ukiwa na maswali yoyote yanayohusiana na Kitovu cha WhatsApp cha Habari kuhusu Virusi vya Korona, wasiliana nasi.