1. Pakua na uzindue Programu ya WhatsApp Business: programu ya WhatsApp Business inaweza kupakuliwa bila malipo kwenye Duka la Google Play na Duka la Programu la Apple. Gusa ikoni ya WhatsApp Business kwenye skrini yako ya nyumbani.
2. Kagua Masharti ya Huduma: Soma Masharti ya Huduma ya WhatsApp Business, kisha gusa Kubali na Endelea ili kukubali masharti hayo.
3. Jisajili: Chagua nchi yako kutoka kwenye orodha kunjuzi ili uongeze msimbo wa nchi yako, kisha uingize nambari yako ya simu kwa mfumo wa kimataifa wa nambari ya simu. Gusa Imekamilika au Endelea, kisha gusa Sawa ili upokee msimbo wako wa kusajili wa tarakimu 6 kupitia SMS au kwa kupigiwa simu. Ili kukamilisha usajili, ingiza msimbo wako wa tarakimu 6. Jifunze jinsi ya kusajili nambari yako ya simu kwenye makala haya.
4. Toa ruhusa ya kuweza kufikia anwani na picha: Anwani zinaweza kuongezwa kwenye programu ya WhatsApp Business, kutoka kwenye kitabu chako cha anwani. Pia, unaweza kutoa ruhusa ya kufikia picha, video na faili zilizo kwenye simu yako.
5. Unda akaunti: Jaza jina la biashara yako, chagua aina ya biashara, na uchague picha ya jalada.
6. Unda jalada lako la biashara: Gusa GUNDUA > Jalada la biashara. Hapa, unaweza kuongeza habari muhimu za biashara kama anwani yako ya biashara, maelezo, saa na mengineyo.
7. Anza kupiga gumzo. Sasa jalada la biashara yako limesanidiwa. Gusa au , kisha utafute au uchague mtu wa kutumia ujumbe. Andika ujumbe kwenye sehemu ya matini. Kisha, gusa au .
Programu ya WhatsApp Business ina zana kadhaa za kukusaidia kuendesha biashara yako kwa ufanisi. Ili kugundua zana hizi, nenda kwenye skrini ya soga zako. Gusa Chaguo Zaidikwenye Android au Mipangilio kwenye iPhone. Kisha, gusa Zana za Biashara.