Endelea kuunganishwa na jamii yako
Unda kiungo kifupi ambacho wateja wanaweza kutumia kuanzisha soga ya WhatsApp nawe. Shiriki kiungo kwa barua pepe, tovuti yako, ukurasa wa Facebook, au njia zingine zitumikazo mara kwa mara.
Wakati huu wa kutokuwa na uhakika na kujitenga, ungana na jamii yako kwenye WhatsApp—chombo kilekile wanachotumia kuwa karibu na marafiki na familia.
Tafadhali tumia WhatsApp kwa njia nzuri unapowasiliana na wateja wako. Wasiliana tu na watumiaji unaowajua wanaotaka kupokea ujumbe kutoka kwako, waombe wateja wahifadhi nambari yako ya simu kwenye vitabu vyao vya anwani na ujiepushe na kutuma ujumbe wa kiotomati au matangazo ya biashara kwa vikundi. Kwa kutofuata maadili bora ya kimsingi kunaweza kusababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine na uwezekano wa akaunti kupigwa marufuku.
Ili kudhibiti vyema maswali mengi, angazia taarifa yenye manufaa katika jalada la biashara na ushiriki maelezo kuhusu huduma zako kwenye katalogi, tunapendekeza utumie programu ya WhatsApp Business, unayoweza kupakua bila malipo. Bofya hapa ili upate mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Programu ya WhatsApp Business. Kama unataka kuhamisha akaunti yako kutoka kwa WhatsApp Messenger kuenda kwa programu ya WhatsApp Business, bofya hapa.
Pakua kwa simu yako
Unda kiungo kifupi ambacho wateja wanaweza kutumia kuanzisha soga ya WhatsApp nawe. Shiriki kiungo kwa barua pepe, tovuti yako, ukurasa wa Facebook, au njia zingine zitumikazo mara kwa mara.
Jaza wasifu wako wa biashara na usanidi ujumbe maalum wa salamu ili watu wajue mahali wanapoweza kupata rasilimali na maelezo zaidi kuhusu huduma zako.
Wakati huu ambapo kuna shughuli nyingi, fahamisha jamii yako ijue wakati wa kutarajia majibu kutoka kwako kwa kutumia ujumbe otomatiki wa kuwa mbali.
Elimisha jamii yako kuhusu huduma wanazoweza kupata. Jumuisha maelezo ya huduma kwenye katalogi yako, inayopatikana kupitia jalada lako la biashara.
Hifadhi na utumie tena ujumbe unaotuma mara kwa mara ili uweze kujibu kwa haraka maswali ya wanajamii.
Taarifu na uelimishe jamii yako kwa dhati kuhusu jinsi wanavyoweza kusaidia katika kupunguza uenezaji wa virusi. Tumia picha, video na maandishi kuonyesha vidokezo kwenye sasisho la hali.
Tumia vikundi na simu za video za vikundi kushirikiana na timu yako kwa mbali.
Tumia WhatsApp Web kudhibiti idadi kubwa ya ujumbe wa WhatsApp kwa njia ya haraka na rahisi kwa kutumia kompyuta yako ya dawati.
Ukiwa na maswali yoyote yanayohusiana na Kitovu cha WhatsApp cha Habari kuhusu Virusi vya Korona, wasiliana nasi.