
Wakati huu wa kutokuwa na uhakika na kutengwa, unaweza kuwasiliana na wagonjwa wako na wafanyakazi wenza kwenye WhatsApp—chombo kilekile wanachokitumia kukaa karibu na marafiki na familia.
Tafadhali tumia WhatsApp kwa njia nzuri unapowasiliana na wateja wako. Wasiliana tu na watumiaji unaowajua wanaotaka kupokea ujumbe kutoka kwako, waulize wateja wahifadhi nambari yako ya simu kwenye vitabu vyao vya anwani na ujiepushe na kutuma ujumbe wa kiotomati au matangazo ya biashara kwa vikundi. Kwa kutofuata maadili bora ya kimsingi kunaweza kusababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine na labda kwa akaunti kupigwa marufuku.
Ili kudhibiti vyema maswali mengi, onyesha taarifa zenye manufaa kama vile saa za kazi na uhifadhi majibu yanayotumiwa mara kwa mara, tunapendekeza utumie programu ya WhatsApp Business, unayoweza kupakua bila malipo. Bofya hapa ili upate mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Programu ya WhatsApp Business. Kama unataka kuhamisha akaunti yako kutoka kwa WhatsApp Messenger kuenda kwa programu ya WhatsApp Business, bofya hapa.
Pakua kwa simu yako
Ikiwa bado huna nambari za simu za wagonjwa wako, unda kiungo kifupi ambacho wagonjwa wanaweza kukitumia kuanza kupiga soga ya faragha kwenye WhatsApp nawe. Shiriki kiungo kupitia barua pepe, ukurasa wako wa Facebook, au njia nyingine zisizo za umma.
Unaweza kuweka ujumbe maalum wa salamu ili wagonjwa wapate habari na rasilimali ya mara moja, wanapowasiliana nawe.
Tumia orodha ya tangazo kutuma ujumbe sawa wa faragha kwa watu kadhaa unaowasiliana nao kwa wakati mmoja. Watu waliokuongeza kwenye vitabu vyao vya anwani pekee ndio watapokea ujumbe wa tangazo lako.
Tumia video na simu za sauti zilizofumbwa kuwasiliana na wagonjwa au wafanyakazi wenza ambao huenda ikawa vigumu kuwasiliana nao ana kwa ana.*
Hifadhi na utumie tena ujumbe unaotuma mara kwa mara ili uweze kujibu kwa haraka maswali ya wagonjwa.
Kwa kutumia hali, unaweza kuchapisha maandishi, picha na masasisho ya video. Shiriki vidokezo kuhusu mazoea bora ya usafi na njia zingine za kupunguza kuenea kwa virusi.
Hakikisha kuwa wagonjwa wako wanajua wakati unapopatikana, hasa kama umebadilisha saa zako za kazi ili uweze kushughulikia mahitaji ya sasa ya ndani.
Wakati huu ambapo kuna shughuli nyingi, wafahamishe wagonjwa wako wajue wakati wa kutarajia majibu kutoka kwako kwa kutumia ujumbe otomatiki wa kuwa mbali.
Tumia vikundi na simu za video za kikundi kushiriki masasisho yanayohusu mkurupuko wa hivi karibuni.
*Ni wajibu wa kila mtumiaji wa WhatsApp kuhakikisha kuwa matumizi yoyote ya WhatsApp yanazingatia sheria husika, ikiwa ni pamoja na faragha ya data ya huduma ya afya na sheria za usalama. WhatsApp haipangi wala kutoa huduma za afya wala huwezi kudai kuwa WhatsApp inahusiana na shughuli zako za utoaji wa huduma ya afya. WhatsApp sio mbadala wa mashauri ya afya ya kibinafsi kwa wagonjwa au kwa matibabu ya hali ambazo zinahitaji matibabu ya haraka, haitatumika kama utaratibu wa kifaa cha matibabu kilichodhibitiwa.
Ukiwa na maswali yoyote yanayohusiana na Kitovu cha WhatsApp cha Habari kuhusu Virusi vya Korona, wasiliana nasi.