Ungana kwa mbali
Tumia vipengele vya WhatsApp, kama vikundi, sauti na simu za video ili kuendelea kuungana na kutoa msaada kwa wapendwa hata kama hampo mahali pamoja.
WhatsApp inakusaidia kujiunga na wale ambao ni muhimu zaidi kwako. Hizi hapa ni baadhi ya njia unazoweza kutumia WhatsApp kuwatunza marafiki na familia, kupata habari rasmi za afya za hivi punde na kushiriki habari kwa umakinifu. Ikiwa hujawahi kutumia WhatsApp au unataka tu kujikumbusha jinsi ya kutumia, huu hapa ni mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuanza kutumia WhatsApp.
Tumia vipengele vya WhatsApp, kama vikundi, sauti na simu za video ili kuendelea kuungana na kutoa msaada kwa wapendwa hata kama hampo mahali pamoja.
Ungana na mashirika ya ndani, ya kitaifa na ya kimataifa. Tumia vyanzo vinavyoaminika, kama Shirika la Afya Duniani au wizara ya afya ya kitaifa kwa habari na miongozo ya hivi karibuni.
Fikiria kuhusu ujumbe unaopokea, kwani si kila kitu unachotumiwa kuhusu virusi vya korona kinaweza kuwa sahihi. Thibitisha ukweli kwenye vyanzo vingine rasmi vya kuaminika, wakaguzi wa ukweli au kupitia programu ya gumzo ya kuangalia ukweli ya International Fact-Checking Network (IFCN) katika +1 (727) 2912606. Ikiwa huna uhakika na jambo fulani, usilisambaze.
Tumejitolea kuwapa viongozi wa jamii msaada mkiwa mnapambana na changamoto hili. Jifunze jinsi unavyoweza kutumia WhatsApp kutaarifu na kuungana na jamii yako wakati watu wana wasiwasi kuhusu virusi vya korona.
Jifunze jinsi unavyoweza kuungana na wagonjwa wako, kutaarifu jamii, kuandaa mikutano kwa mbali, kuweka majibu ya haraka kwa maswali yanayoulizwa sana na zaidi.
Jifunze namna ya kuungana na wanafunzi wako kwenye WhatsApp, kutuma na kupokea kazi, kushiriki masomo katika muundo wa maandishi na ujumbe wa sauti na zaidi.
Litambulishe shirika lako, endelea kuungana na jamii yako, shiriki habari sahihi na kwa wakati muafaka, shirikiana na timu yako, jibu maswali ya kawaida kwa haraka na zaidi.
Tafuta njia zaidi za kuendelea kuungana na wateja wako, shiriki saa zako za sasa za biashara, fanya iwe rahisi kujichukulia na kuletewa bidhaa, toa taarifa za mara kwa mara za bidhaa zilizopo na zaidi.
Tazama jinsi watu wanavyotumia WhatsApp kuwasiliana na jamii zao wakati huu mgumu:
Nchini Pakistan, kikundi fulani cha WhatsApp kilikusanya Rs milioni 21 za kuwasaidia walio wanyonge katika jamii dhidi ya kuathirika sana na umasikini: Soma makala hayo hapa >
Kundi la Mameya wa Kiitaliano waliendelea kuungana kwa kutumia WhatsApp: Soma makala hayo hapa >
Shule za msingi jijini Naples, Italia zinaendelea na masomo licha ya kufungwa, kwa kutumia WhatsApp kutuma kazi kwa familia: Soma makala hayo hapa >
Mtu fulani nchini Hong Kong anatumia WhatsApp kuishawishi jamii yake kusaidia biashara za ndani: Soma makala hayo hapa >
Mpango fulani wa kuwezesha kupata kazi nchini Jordan unatumia WhatsApp kuendelea kuwatia moyo wanawake watafute kazi wakati makali ya Virusi vya Korona yanapoongezeka: Soma makala hayo hapa >
Wataalamu wa Afya huko Paris wameanzisha kikundi cha WhatsApp ili kupata habari za hivi punde kuhusu idadi ya wagonjwa hospitalini: Soma makala hayo hapa >
Maofisa wa Coimbatore, nchini India hufanya mikutano kupitia WhatsApp: Soma makala hayo hapa >
Walimu kwenye kambi za wakimbizi nchini Syria wanashiriki video za mafunzo na wazazi kwa kutumia WhatsApp: Soma makala hayo hapo >
Manusura wa utumwa nchini India wanatumia vikundi vya WhatsApp kuwaelimisha wenzao kuhusu virusi vya korona: Soma makala hayo hapa >
Wagonjwa walio Florianópolis, nchini Brazil wanaweza kupanga miadi na kuuliza maswali kwa kutumia WhatsApp: Soma makala hayo hapa >