Shiriki picha, video, madokezo ya sauti na maandishi na watu wako kwenye Hali ya WhatsApp. Binafsisha kwa kuongeza vibandiko, GIF na zaidi. Yatapotea kwenye mwonekano baada ya saa 24.
Kwa vibandiko, avata, GIF na maandishi tandazo, una chaguo zote za ubunifu kiganjani mwako ili kuweza kujieleza, kuwa mbunifu na kushiriki uhalisi wako.
Endelea kujulisha kila mtu unayempenda na umtaje katika hali yako wakati una kitu ambacho ungependa aone. Anaweza kuipenda na kuijibu ili kuanzisha mazungumzo.
Hali yako ni yako ya kushiriki. Ukichapisha, unaamua ni nani anayeweza kuiona, kwa hivyo unaweza kushiriki matukio yako ya nyuma ya pazia kwa amani ya ziada ya kiakili.