Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Kutumia mifumo ya kidijitali hutoa fursa nyingi za kuboresha maisha yetu, lakini ni muhimu kufahamu hatari zilizopo ili uweze kujilinda wewe na Jumuiya yako. Jifunze jinsi ya kuwaweka wanajumuiya wako salama na kulinda faragha yao kwa kudhibiti Vikundi na mazungumzo na kuwahimiza wanajumuiya kutumia Vipengele vya Usalama na Faragha vya Whatsapp.
"Katika hali ya kuwasaidia wahasiriwa wa unyanyasaji wa nyumbani, ambayo ilibidi kushughulikiwa kwa faragha sana, msimamizi wa kikundi aliona WhatsApp ikiwa imesimbwa kwa njia fiche kutoka mwisho hadi mwisho na alijiamini zaidi kuwa na majadiliano hayo kwenye programu. Ni muhimu kuwa faragha ni ya hali ya juu na chochote unachojadili hakishirikiwi na hadhira isiyotarajiwa."
- Givers Arena, Nigeria
Wakati watu wanahisi salama katika jumuiya, kuna uwezekano mkubwa wa kushiriki na kuhisi kukubalika. Hisia hiyo hupotea haraka sana ikiwa washiriki watawekwa kwenye hatari ya maudhui au tabia mbaya, wakati Kikundi hakihisi kuwa cha faragha, au wakati maelezo ya kibinafsi yanaposhirikiwa bila idhini.
Usalama ni muhimu sana katika utendaji wa WhatsApp. Ujumbe wako wa kibinafsi, picha, video, ujumbe wa sauti, hati na simu zinalindwa kwa usimbaji fiche kutoka mwisho hadi mwisho. Tumia vipengele vya usalama na faragha kwenye WhatsApp ili kujilinda wewe na wanajumuiya wako. Kama msimamizi wa Jumuiya, ni muhimu kushirikiana na wasimamizi wa Vikundi ili kuhakikisha wanajumuiya wako salama.
Wanajumuiya wa Jumuiya za WhatsApp wanaweza kupata kwa urahisi maelezo ya mawasiliano ya wasimamizi wa Vikundi vyao na wanaweza kufikia wasimamizi wa Jumuiya zao moja kwa moja ikiwa watahitaji.
Usiweke Jumuiya za WhatsApp ambazo:
Kama msimamizi wa Jumuiya, unakubali kutumia Huduma zetu kwa mujibu wa Masharti yetu ya Huduma. Hatua inaweza kuchukuliwa kuhusiana na akaunti yako, ikiwa ni pamoja na kuzima au kupiga marufuku Jumuiya, iwapo kuna ukiukaji.
Hakikisha kila mmoja anafahamu vipengele vya usalama na faragha vinavyotolewa na WhatsApp ili kuwalinda watumiaji dhidi ya wadukuzi. Wasimamizi wa Jumuiya na Vikundi wanapaswa kuangalia mtu yeyote anayejaribu kuchukua akaunti yako, kushiriki maelezo ya uwongo au kuongeza au kuondoa wanajumuiya. Unapaswa kuwahimiza wanajumuiya walinde akaunti zao, na uwakumbushe wasishiriki na watu wengine maelezo ya Jumuiya ili kuzuia kuhatarisha Jumuiya. Kama msimamizi wa Jumuiya, unaweza kuondoa wanajumuiya, kufuta ujumbe usiokuwa muhimu (kwa hadi siku 2.5 baada ya kutumwa) ili kuweka jumuiya salama.
Jilinde wewe na wanajumuiya wako kwa kuwaeleza umuhimu wa:
Wakumbushe wanajumuiya wako kwamba wanaweza kutumia vipengele vya ziada vya faragha, kama vile jumbe zinazotoweka na midia ya kutazama mara moja, wakati wowote wanaposhiriki maelezo ya kibinafsi ndani ya Vikundi. Wahimize wanajumuiya wote kutumia zana na vipengele ambavyo tumeunda ili kuhakikisha usalama na faragha yako.
Kwa wasimamizi wa Jumuiya, ni muhimu sana kuwa mwangalifu unapotuma ujumbe kwenye kikundi cha Matangazo. Usimtaje yeyote katika kikundi cha Matangazo, kwa kuwa kufanya hivyo kutaonyesha nambari ya simu ya mtu huyo kwa jumuiya nzima.
Jumuiya za WhatsApp hutoa safu ya ziada ya faragha kwa kuwa watumiaji hawawezi kutafuta hadharani mtandaoni kwa ajili ya jumuiya yako, lakini lazima waalikwe ili wajiunge. Shirikiana na wasimamizi wa jumuiya yako na wa Vikundi ili kuhakikisha wanajumuiya wanaoongezwa kwenye jumuiya kwa sababu mwafaka. Kuwepo kwa washiriki wenye nia mbaya au wasiofahamu lengo la jumuiya huenda kukaathiri ufaafu wa jumuiya, au kunaweza kuhatarisha jumuiya kupitia unyanyasaji, ulaghai au madhara mengine.
Ni muhimu kwako kusimamia na kudhibiti kikamilifu jinsi Vikundi na wanajumuiya hujiunga na kuingiliana na Vikundi vingine kwenye jumuiya yako. Kila jumuiya inaweza kuwa na Vikundi hamsini pamoja na Kikundi cha Matangazo, kwa hivyo angalia uundaji mpya wa Kikundi ili kuhakikisha kuwa Vikundi vinavyohusika pekee ndivyo vimeunganishwa kwenye Jumuiya yako.
Hakikisha wasimamizi wa Kikundi chako wanafuatilia washiriki wapya na kuondoa mtu yeyote ambaye hapaswi kuwepo. Unaweza kuwaondoa wanajumuiya kwa kwenda katika orodha ya washiriki wa Kikundi na kubofya jina la mwanajumuiya huyo.
Unaalika Vikundi na wanajumuiya kujiunga na jumuiya kwa kutumia viungo vya mwaliko au kwa kuongeza watumiaji kwenye anwani zako kibinafsi. Kuwa mwangalifu unaposhiriki viungo vya mwaliko. Kamwe usichapishe viungo hivi kwenye tovuti za umma. Tuma viungo vya mwaliko kwa faragha kwa watu unaowajua pekee. Unaweza pia kuwasha mipangilio ya ombi la kujiunga na kikundi kwa vikundi ambavyo vitahitaji wasimamizi wakague washiriki wowote wapya kabla ya kujiunga na kikundi. Ukimwongeza mtu kisha ajiondoe, heshimu uamuzi wake.
Hakikisha wasimamizi wote wanafahamu wajibu wao na wamefunzwa kuweka Vikundi vyao salama. Chunguza migogoro, unyanyasaji, uonevu na maudhui hatari, na utekeleze sheria za jumuiya yako ifaavyo. Futa haraka ujumbe usiofaa au usioaminika kwa kubofya na kushikilia ujumbe huo, kisha ikihitajika, zuia, ripoti, na uondoe Vikundi na wanajumuiya wanaokiuka kanuni.
Wasaidie wasimamizi na wanajumuiya kutambua maudhui yasiyoruhusiwa, kulingana na kanuni za jumuiya na matarajio ya washiriki. Maudhui yasiyoruhusiwa kwenye jumuiya yako ni yale:
Wakumbushe wanajumuiya kupuuza maudhui au kuripoti vitendo vya kutiliwa shaka, na kuwa makini kabla ya kusambaza ujumbe.
WhatsApp inazuia usambazaji wa ujumbe ili kupunguza kasi ya kuenea kwa habari potofu. Unaweza kusambaza ujumbe kwa gumzo tano kwa wakati mmoja. Ikiwa ujumbe tayari umesambazwa, unaweza kuusambaza kwenye hadi soga tano, ikiwa ni pamoja na kwenye kikundi kimoja.
Ukiona maudhui au tabia inayokuhusu, au ikiwa mtu yeyote katika jumuiya yako yuko hatarini, mfikie kwa usaidizi mara moja. Wasiliana na huduma za dharura za eneo lako, watekelezaji sheria au nambari ya dharura ya kuzuia kujiua.
Kuhusu barua taka na ujumbe usiotakikana
Kuhusu vikomo vya kusambaza
Wasimamizi wa jumuiya wana jukumu muhimu katika kudhibiti na kudumisha Jumuiya za Whatsapp. Fahamu unachohitaji ili kuweza kusimamia jumuiya ipasavyo.