"Tulijaribu kupunguza matatizo kwa kurejelea miongozo ya jumuiya yetu kila mara na kuanzisha vikundi vya dharura kwa ajili ya kutatua migogoro. Hivi ni muhimu sana katika kushughulikia maswala nyeti."
- Yohana, Indonesian Babywearers
Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Kuunda jumuiya salama huanza kwa kuandika sheria zilizo wazi, mahususi na zinazoweza kutekelezeka. Fahamu jinsi ya kuhakikisha kuwa wanachama wanajua la kufanya wanapokabiliwa na maudhui yenye matatizo au watu na jinsi ya kutekeleza sheria za jumuiya kwa uwazi na kwa uthabiti.
"Tulijaribu kupunguza matatizo kwa kurejelea miongozo ya jumuiya yetu kila mara na kuanzisha vikundi vya dharura kwa ajili ya kutatua migogoro. Hivi ni muhimu sana katika kushughulikia maswala nyeti."
- Yohana, Indonesian Babywearers
Sheria nzuri zinaonyesha maadili ya jamii. Zinabainisha tabia zinazokubalika na zisizokubalika. Pia zinaeleza kwa uwazi ni hatua gani zitapelekea onyo, kuondolewa au kuripoti kwa WhatsApp.
Wanajumuiya watafaidika kwa kujua jinsi wanavyoweza kutoa maoni, nini cha kufanya wakati mwanajumuiya anakiuka sheria na jinsi wanavyoweza kuwasiliana na wasimamizi ikiwa wana wasiwasi wowote. Ni vyema kujumuisha kiungo cha Sheria na Masharti ya WhatsApp katika sheria za jumuiya yako.
Kama msimamizi una jukumu la kulinda jumuiya yako. Wanajumuiya wanaangalia uongozi wako wakati kanuni za jumuiya haziheshimiwi. Wanakutarajia ufuate sheria mara kwa mara na kuondoa maudhui na wanachama wanaokiuka sheria hizo.
Wahimize washiriki kuchukua hatua wakati wanakabiliwa na maudhui na/au watu wenye matatizo:
Ikiwezekana, wasimamizi wa jumuiya wanapaswa kufanya kazi na wasimamizi wa Kikundi na wanajumuiya ili kudhibiti na kutatua masuala katika ngazi ya Kikundi. Ukichagua kuripoti tabia au maudhui yenye matatizo kwa WhatsApp, unaweza kuripoti ujumbe na akaunti mahususi kwa kubonyeza ujumbe kwa muda mrefu. Kuripoti ujumbe hakuhusishi akaunti nyingine au maudhui ya jumuiya yako.
Matamshi ya chuki, vurugu, ponografia, au ujumbe mwingine usiotakikana au wenye madhara unaokiuka sheria za jumuiya unapaswa kufutwa mara moja ili kuzuia maudhui yasionekane na wanajumuiya wengi. Ni muhimu kuwasiliana haraka na kuchunguza chanzo ili kubaini nia yao.
Usisite kumwondoa mwanajumuiya kwenye Kikundi au jumuiya ikiwa kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria zako. Ukimwondoa mwanajumuiya anayejulikana sana, zingatia kutuma ujumbe mfupi unaoeleza kuwa mtu huyo si sehemu ya Jumuiya tena. Jihadhari usifichue maelezo yoyote nyeti ya kibinafsi yanayohusiana na hali hiyo au wanajumuiya wanaohusika.
Shirikiana na wasimamizi na wanajumuiya kutambua wazushi na wasumbufu. Mwenye matusi hukusudia kuleta utata na kwa kawaida hujitambulisha kwa utambulisho bandia na kuwa na tabia ya kutatiza. Waharibifu ni watu wanaochukua Kikundi chako kwa kubadilisha picha ya Kikundi chako kwa mfano. Ondoa wenye matusi kwa haraka na waharibifu au wanachama wanaokiuka sheria za jumuiya.
Haijalishi ni hatua gani unachukua, ni wazo nzuri kutaja upya sheria katika kikundi cha Matangazo, na kuwafahamisha wanajumuiya wote ulichofanya kutatua suala hilo.
Wanajumuiya wanakutegemea udumishe usalama wa jumuiya. Usiruhusu watu kutenda isivyofaa, kukutisha wewe, au kujaribu kukuzuia kufanya jambo sahihi. Unaweza kumzuia mwanajumuiya anayewasiliana nawe baada ya kuondolewa au anayejaribu kukuzuia kumwondoa kwenye Kikundi au jumuiya.
Baada ya kuzuiwa, ujumbe, simu na masasisho ya hali yanayotumwa na mwanajumuiya wa zamani hayataonekana kwenye simu yako na hayatafika kwako. Mara ya mwisho kuonekana, mtandaoni, masasisho ya hali na mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwenye picha yako ya wasifu hayataonekana tena kwa watu waliozuiwa.
Ukiripoti mwanajumuiya, WhatsApp inaweza kupiga marufuku akaunti yake ikiwa tunaamini kuwa amekiuka Sheria na Masharti yetu. Wahimize wanajumuiya wasome kwa uangalifu sehemu ya “Matumizi Yanayokubalika ya Huduma Zetu” kwenye Sheria na Masharti yetu ili wapate maelezo zaidi kuhusu utumiaji wa WhatsApp, na ukiukaji wa Sheria na Masharti yetu unaoweza kusababisha akaunti kupigwa marufuku.
Akaunti ikipigwa marufuku, mtumiaji ataona ujumbe ufuatao anapojaribu kufungua WhatsApp – "Nambari yako ya simu imepigwa marufuku kutumia WhatsApp. Wasiliana na Usaidizi ili kupata msaada." Ikiwa mtumiaji anafikiri akaunti yake ilipigwa marufuku kimakosa, anaweza kuwasiliana na WhatsApp na kesi itafunguliwa.
Ikiwa kuna hali ya dharura, au ikiwa una wasiwasi kuwa mwanajumuiya ni hatari kwake mwenyewe au kwa wengine, wasiliana na huduma za dharura za eneo lako au nambari ya simu ya kuzuia kujiua mara moja. Ukipokea au ukikumbana na maudhui yanayoonyesha mtoto akinyanyaswa au akidhulumiwa, wasiliana na Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) au Kituo cha Kimataifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (ICMEC), kisha umripoti na umzuie mtumiaji husika. Usiwahi kusambaza maudhui ya matusi kwa wengine, hata kwa mtindo wa kulaani, unapotuma ujumbe kuhusu tukio hilo.
Wasimamizi wa jumuiya wana jukumu kubwa la kusimamia na kukuza jumuiya kwa usalama. Fahamu jinsi ya kutambua na kuunda timu dhabiti ya wasimamizi, kugawana majukumu, na kutayarisha michakato ya kuwasaidia kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi.