"Tunataka kupunguza idadi ya wanajumuiya katika jumuiya yetu ili kuhakikisha kwamba wanajumuiya wetu wanashiriki na kujitolea kwa ajili yetu kudumisha ari ya kikundi."
- Karlina, BTS Army
Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Kuweka na kufahamisha kuhusu mipaka iliyo wazi tangu mwanzo huwasaidia washiriki kuingiliana kwa usalama na vyema. Fahamu jinsi unavyoweza kushirikiana na wanajumuiya ili kudumisha uhusiano mwema kwa kuwaelimisha kuhusu habari potofu, ulaghai na jinsi ya kukabiliana na uonevu na unyanyasaji. Utakuwa unawapa maarifa na uwezo wa kuunda aina ya jumuiya jumuishi ambayo watataka kuwa sehemu yake.
"Tunataka kupunguza idadi ya wanajumuiya katika jumuiya yetu ili kuhakikisha kwamba wanajumuiya wetu wanashiriki na kujitolea kwa ajili yetu kudumisha ari ya kikundi."
- Karlina, BTS Army
Kushiriki katika jumuiya kunapaswa kufurahisha na kuthawabisha lakini kunaweza kuwa na usumbufu kwa hivyo wasimamizi wa jumuiya na Kikundi lazima washirikiane ili kudumisha mazingira mazuri. Vifuatavyo ni vidokezo vya kusaidia jumuiya yako kukuza desturi ya kuheshimiana.
Mipaka inafafanua wazi tabia salama na inayokubalika. Inafafanua kile tunachostarehekea au kutoridhika nacho, na jinsi tungependa kutendewa na wengine. Mipaka hufafanua majukumu na matarajio na kusaidia kujenga uaminifu. Unapoandika sheria za jumuiya yako, tumia toni nzuri ili kuwasilisha mipaka hii na ni hatua gani utachukua sheria zikivunjwa.
Jumuiya zilizo na utamaduni mzuri na migogoro michache huthamini mafanikio yao kwa sheria nzuri zilizowasilishwa kwa uwazi siku ya kwanza. Chapisha sheria zako katika maelezo ya jumuiya ili ziwe maarufu na zipatikane kwa urahisi, na uzitangaze mara kwa mara katika Kikundi cha Matangazo. Ni muhimu kubadilisha ipasavyo sheria kadri jumuiya yako inavyozidi kukua na kubadilika ili kuhakikisha zinafaa wanajumuiya wote. Hakikisha unawasilisha vyema na kwa uwazi matarajio au mabadiliko yoyote mapya, na anzisha mabadiliko ya sheria hatua kwa hatua ili kuruhusu jumuiya yako kujibu na kuzoea.
Kwa ustawi wako mwenyewe ni muhimu kuzingatia mipaka yako ya kibinafsi na kuweka matarajio wakati kuna upatikanaji. Kwa mfano, unaweza kutaka kuweka saa zako za mtandaoni kuanzia saa 3 asubuhi - saa 12 jioni, Jumatatu hadi Ijumaa, ili kufahamisha timu yako ya msimamizi na wanachama kuwa hutajibu ujumbe nje ya muda huu.
Fanya kazi na wasimamizi wa Kikundi ili kuangalia ukiukaji wa sheria za jumuiya yako, na taarifa na mwingiliano unaoweza kudhuru ndani ya vikundi vyako. Chukua hatua mara moja ili kuzima mazungumzo yasiyotakikana au yenye madhara na kuyazuia kuenea. Ni muhimu kufuta haraka ujumbe unaokiuka matarajio na sheria za jumuiya yako. Unaweza pia kufikiria kubadilisha kwa muda mpangilio wa kikundi wa "Tuma Ujumbe" hadi "Wasimamizi Pekee" ili kuzuia washiriki kutuma ujumbe zaidi ikiwa mazungumzo ya Kikundi yamekuwa mabaya.
Habari potofu mara nyingi huenea sana. Hata ikiwa ujumbe umeshirikiwa mara nyingi, haimaanishi ni wa kweli. Picha, video na rekodi za sauti zinaweza kuhaririwa ili kuwapotosha watu.
Wahimize wanakikundi wakague kila wakati ujumbe wa kutiliwa shaka au unaoleta wasiwasi ili kuhakikisha ni wa kweli na waepuke taarifa za uongo kwa kufanya yafuatayo:
Ni busara hasa kuangalia mara mbili ukweli katika ujumbe ulioandikwa "Ujumbe Uliosambazwa Sana," kwa kuwa ziko umbali wa angalau kusambazwa mara tano kutoka kwa mtumaji asili.
Wakumbushe wanajumuiya kwamba habari ambazo ni ngumu kuamini mara nyingi huwa si za kweli. Ujumbe na viungo vingi vya ulaghai vina makosa ya tahajia au sarufi, au vina ombi kwa mpokeaji kushiriki maelezo ya kibinafsi. Daima "wekelea kishale" juu ya kiungo na uangalie kwa makini kabla ya kukibofya.
Ukiona jumbe zilizo na taarifa za uwongo, mjulishe haraka mtumaji kwamba taarifa hiyo si sahihi. Mweleze arekebishe na afafanue ujumbe huo kwenye kikundi mara moja. Ikiwa mwanajumuiya mara kwa mara anashiriki habari za uwongo, wasiliana naye kwa faragha ili ueleze ni kwa nini hii ni hatari na umsaidie kuelewa jinsi ya kutambua habari potofu. Usichelewe kuwaondoa wakosaji wakubwa kutoka kwa Kikundi au jamii.
Uonevu ni wakati mtu ananyanyasa, kutishia, kumwaibisha, au kumlenga mtu mwingine kwa nia ya kumdharau au kumwaibisha. Fanya kazi na wasimamizi wako ili kuangalia ishara hizi za matumizi mabaya:
Wakati mwanajumuiya anamdhulumu au kumnyanyasa mwingine, chukua hatua haraka ili kufuta ujumbe au maudhui yoyote ambayo yanakiuka sheria za jumuiya. Wasiliana na mwanajumuiya aliyekosea ili kumkumbusha matarajio ya jumuiya, na kufafanua na kutuliza hali hiyo. Unaweza kujaribu kupata ufahamu wa kina wa kile kilichosababisha uonevu au unyanyasaji mwanzoni, ili kumsaidia kuelewa jinsi kitendo chake kilimfanya mwanajumuiya mwingine kuhisi na athari kwa Kikundi na jumuiya. Hakikisha anaelewa matokeo ya tabia zake au waulize wanajumuiya maoni yao kuhusu jinsi ya kutatua tatizo na kujenga upya uaminifu. Au unaweza kutaka kumpiga marufuku mkosaji kutoka kwa jumuiya.
Pia ni muhimu kumfikia mwathirika na kutoa faraja na usaidizi. Wakumbushe kuwasiliana na wasimamizi au watu wanaowaamini ili kupata usaidizi na waeleze kuwa wanaweza kudhibiti mwingiliano wao kwa kumzuia mwanajumuiya.
Wakati unachunguza na kuzungumza na washiriki wanaohusika unaweza kutaka kuwaomba wasimamizi wa Kikundi kunyamazisha Kikundi chao kwa muda kwa kurekebisha mipangilio ili kuruhusu wasimamizi pekee kutuma ujumbe.
Iwapo mwanajumuiya ana uhasama kila mara na anaonea na kuwanyanyasa wengine, unapaswa kumwondoa mara moja kutoka kwa Jumuiya na kutoka kwa kila Kundi analoshiriki.
Usalama wa jumuiya ni jukumu la watu wote. Jadili kwa uwazi madhara yanayoweza kutokea mtandaoni na uunde utamaduni ambapo wanajumuiya wanahisi hisia kali ya kukubalika na wajibu kwa ajili ya ustawi wa jumuiya.
Shiriki vidokezo na maelezo kuhusu usalama mtandaoni kwa bidii ili kuwasaidia wanajumuiya kuelewa jinsi ya kujilinda wao wenyewe na wengine dhidi ya hatari zozote. Pia, hakikisha kuwa wanachama wanajua kuhusu mipangilio ya faragha na usalama inayowasaidia kukaa salama wanapotumia WhatsApp.
Tumia sheria za jumuiya yako kuunda mazingira mazuri na jumuishi yanayothamini na kukubali tofauti za maoni, na kuhimiza heshima kwa wengine ndani ya jumuiya. Kuwasaidia wanajumuiya kuelewa jinsi maneno na matendo yao yanavyowaathiri wengine kunaweza kupunguza unyanyasaji na migogoro.
Wahimize washiriki kuzungumza wanapoona tabia isiyofaa na/au maudhui yanayoelekezwa kwao au kwa mwanajumuiya mwingine. Wanajumuiya wanapofanya majadiliano ya kusisimua yenye maoni na mitazamo tofauti, andika ujumbe kuwashukuru kwa mjadala mzuri.
Migogoro na mizozano mara nyingi hutokana na kutoelewana, na kuwa na mitazamo, maoni na maadili tofauti. Jifunze jinsi ya kudhibiti mizozo, kutatua matatizo kati ya wanajumuiya, na kukuza utofauti na ushirikishwaji katika jumuiya yako.