Kabla hujaanzisha jumuiya, bainisha unalokusudia - je, ni kuratibu na kusimamia mipango ya afya ya umma, kutoa mafunzo na ushauri kwa wahudumu wa afya, kutoa hamasisho kuhusu suala fulani la afya, au kitu kingine? Lengo lako litakusaidia kubainisha wahusika utakaowajumuisha kwenye jumuiya na ni vikundi gani wataingia. Unaweza kuanzisha au kuongeza vikundi vifuatavyo:
- vikundi vya wahudumu wa afya kulingana na eneo la kijiografia;
- vikundi vya wahudumu wa afya kulingana na ujuzi wao;
- vikundi vya wahudumu wa afya kulingana na mpango au matatizo ya afya wanayoshughulikia;
- wahudumu wapya wa afya wanaopokea mafunzo ya msingi;
- mafunzo yanayoendelea ya wahudumu wa afya;
- wasimamizi au waratibu wa mipango;
- timu ya wasimamizi wa hospitali;
- timu za watoa huduma wa afya – madaktari, wauguzi, wahudumu wa afya ya kijamii;
- kikundi cha dawa na vifaa vya matibabu;
- viongozi wa jumuiya.
Kuwa na lengo bayana la jumuiya kutawasaidia wasimamizi wako na wanajumuiya kuelewa sababu za kuongezwa au kutoongezwa kwenye vikundi fulani. Kwa mfano, ikiwa lengo la jumuiya ni kuelimisha kuhusu afya na kutoa huduma muhimu za afya kwa familia, unaweza kuanzisha au kuongeza vikundi vya wataalamu wa masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga, au ushauri nasaha kuhusu afya ya kiakili. Unaweza pia kujumuisha kikundi cha kushiriki mafanikio au kujadili suluhu kuhusiana na changamoto zilizoikabili jamii. Hata hivyo, hufai kujumuisha vikundi visivyohusiana na masuala ya afya kwenye jumuiya yako.