Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Watu hujiunga na jumuiya kupata habari, kuwasiliana na wengine wenye mtazamo sawa, kutiwa motisha, na kushirikiana ili kutimiza lengo moja. Ili kukuza Jumuiya yako ya WhatsApp, unapaswa kuunda nafasi ambayo inakidhi mahitaji ya wanajumuiya wako na kuwezesha miunganisho ya maana na ya kina. Kuwa mbunifu katika kuwasiliana habari na maudhui, na uwahimize washiriki kuhusika, kuingiliana, na kuchangia kwa jumuiya yenye afya, nzuri na inayofanya kazi.
"Kuweza kuunda vikundi vingi na kuvisimamia chini ya mwavuli mmoja kumeleta mguso wa kibinafsi zaidi na kuwezesha kwa kweli kuunda uhusiano wa maana zaidi kati ya wanajumuiya wetu - ambayo ni dhamira yetu yote, kuwaunganisha kila mmoja na kukuza urafiki wa kusaidiana."
- Bruna (International Women Berlin)
Jumuiya hustawi wahusika wanapochangia. Kama msimamizi unaweza kushawishi jinsi washiriki wako wanavyoungana na kuingiliana kwa kuweka usawa unaofaa na kuunda mawasiliano ya mara kwa mara na yenye maana, wala si kuwapatia wanajumuiya maelezo kupita kiasi ambayo yanaweza kuwa taka au kelele.
Hebu tuangalie baadhi ya mawazo ya kukuza na kushirikisha jumuiya yako:
Jumuiya nzuri na yenye kukaribisha huvutia wanajumuiya wapya kujiunga na kuunda mazingira mazuri na ya msaada kwa wote.
Fikiria jinsi utakavyowakaribisha wanajumuiya wapya. Kukaribishwa kwa mtu binafsi katika jumuiya au msimamizi wa Kikundi kunaweza kutia moyo sana. Unapaswa pia kujumuisha maelezo kuhusu madhumuni ya jumuiya, na sheria za kuwasaidia kufahamu jinsi ya kuingia na kushiriki kwa ujasiri.
Wanajumuiya zaidi wanapojiunga, wasimamizi wa jumuiya na Kikundi chako wanaweza pia kusaidia kujenga ushirikiano kwa kuunganisha watu walio na mapendelep yanayofanana. Wakati mwingine, wanajumuiya hawa wapya wanaweza kutaka kuanzisha Kikundi kingine kwenye jumuiya yako.
Ili kuhimiza ushiriki, ni muhimu kwamba wasimamizi wa jumuiya na Kikundi wanapatikana, ni wa kirafiki na wanaoweza kufikiwa. Kuwa mtu wa watu na kushirikiana huwawezesha wanajumuiya kukufahamu na kusaidia kujenga uaminifu. Ukishaimarisha uaminifu, ni rahisi kwa wanajumuiya kuhisi kuwa huru kuja kwako na maswali au kushiriki katika mazungumzo ya Kikundi.
Baadhi ya wanajumuiya huenda wakahitaji maelekezo kuhusu maudhui ya kushiriki au kuzungumzia. Kuuliza maswali rahisi, muhimu, na ya wazi ni njia nzuri ya kutoa majibu na kuongeza ushiriki. Wakati wanakikundi wanajibu , wajibu moja kwa moja ili kuwafahamisha kuwa sauti yao ni muhimu.
Punguza kelele na jumbe za kutatanisha ndani ya Vikundi ili kuwafanya washiriki kupendezwa na kuhusika. Hakikisha matangazo yanaeleweka, yanawahusu wanajumuiya na yanachapishwa kwa wakati unaofaa. Wakumbushe washiriki kutumia kipengele cha "jibu" ili kuweka mazungumzo ya Kikundi kuwa na mpango na yenye mada.
Aina ya maudhui yanayoshirikiwa inategemea madhumuni ya jumuiya yako. Fikiria kuhusu kile ambacho wanajumuiya wako wanatarajia kupata kutoka kwa jumuiya. Ikiwa ni kushiriki habari kuhusu jambo, maudhui ya mara kwa mara kuhusu mada hiyo yatakuwa ya thamani. Ikiwa ni kwa usaidizi wa kijamii, wasimamizi wanaweza kushiriki rasilimali au fursa za kuunganishwa.
Kuwa mbunifu katika jumuiya yako na wasimamizi wa Kikundi. Unaweza kushiriki maudhui kwa njia tofauti kupitia maandishi, video, picha, madokezo ya sauti, GIF, na zaidi. Simu Zilizoratibiwa za Kikundi pia zinaweza kuwa njia mwafaka ya kuhimiza mwingiliano na zinaweza kuwa mabadiliko ya kukaribisha tofauti na ujumbe unaoendelea.
Ni muhimu kuhakikisha Vikundi vinafaa kwa madhumuni. Baada ya muda, zinaweza kuwa kubwa sana kwa kila mtu kupata maudhui sawa kuwa ya maana. Kufanya Vikundi viwe vidogo kwa mambo yanayolengwa zaidi, kunaweza kuimarisha mazungumzo na kukusaidia katika kuamua ni taarifa gani ya kuweka ndani ya Vikundi mahususi na nini cha kutangaza kwa kila mtu.
Jinsi ya kuunda na kushiriki viungo vya kupiga simu
Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti
Ni jambo zuri kutafuta maoni ya mara kwa mara. Fanya kazi na wasimamizi wa Kikundi chako ili kuwauliza washiriki ni aina gani ya taarifa wanayopata kuwa muhimu, au la, na ni nini wangependa kuona zaidi.
Ikiwa ushiriki unashuka ni muhimu kuelewa kwa nini. Je, inaweza kuwa kwa sababu ya maoni mabaya na yasiyo ya heshima, kuenea kwa habari zisizo sahihi, au habari nyingi kupita kiasi?
Wapo wanajumuiya ambao hutoa maoni kila wakati na kushiriki katika soga zote, na pia wapo wanaopendelea kufuatilia mazungumzo yanayoendelea bila kuchangia. Kumbuka kwamba washiriki wasiozungumza bado wanapata thamani kutoka kwa jumuiya yako hata kama hawazungumzi kama wengine.
Ikiwa wanajumuiya wanaondoka kwenye jumuiya, ni vyema kuwauliza ni kwa nini, lakini tafadhali waheshimu wale ambao hawataki kutoa maoni, au kushiriki zaidi.
Mipaka hutoa mwongozo na hubainisha tabia na maudhui yanayokubalika. Fahamu jinsi ya kudhibiti na kuzuia habari potovu, uonevu na madhara mengine.