"Kutenganisha kati ya jumuiya yetu ya wasimamizi na jumuiya ya wanajumuiya kulitusaidia kuratibu vyema wakati wa mizozo."
- Nina, Langsung Enak
Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Ni kawaida migogoro kutokea, na hasa wakati wowote ambapo watu mbalimbali wanatagusana, iwe mtandaoni au ana kwa ana. Pata maelezo kuhusu sababu zinazochochea migogoro mara kwa mara, na jinsi ya kushirikiana na wanajumuiya na timu ya wasimamizi kutatua mizozo inapotokea.
"Kutenganisha kati ya jumuiya yetu ya wasimamizi na jumuiya ya wanajumuiya kulitusaidia kuratibu vyema wakati wa mizozo."
- Nina, Langsung Enak
Watu hujiunga na jumuiya ili kuungana, kupata taarifa, kushiriki hali ya utumiaji, na kujadili na kubadilishana mawazo. Wasimamizi wa jumuiya wanaweza kuzuia migogoro kwa kuunda na kuwasiliana mara kwa mara sheria wazi kuhusu tabia ya wanajumuiya inayokubalika na isiyokubalika, na kutekeleza sheria hizo mara kwa mara na kwa uwazi.
Migogoro ni migumu. Inaweza kutokea wakati watu wanakinzana, au imani na maoni yanapingwa. Inaweza kuwa mawasiliano yasiyofaa, kutoelewana, au kuchanganyikiwa, au kutoka kwa maoni tofauti ya asili juu ya masuala ya sasa au yenye utata. Ni wazo zuri kufanya kazi na timu yako ya msimamizi kuunda mkakati wa upatanishi wa migogoro ili kupunguza, kudhibiti na kutatua mizozo kila mara na kwa njia inayojenga. Angalia migogoro inayoweza kutokea, buni mapema mchakato wa upatanishi na hatua zinazofaa kuchukuliwa ili usaidie timu yako kushughulikia mizozo inapotokea.
Tunapendekeza uwahimize wanajumuiya wako kuwajibika na kuripoti matatizo yoyote kwa timu ya wasimamizi haraka iwezekanavyo, ili uweze kuchukua hatua mara moja ili kupunguza athari mbaya ya migogoro.
Migogoro inapotokea, ingilia haraka ili kupunguza mvutano na uhakikishe:
Linaweza pia kuwa wazo zuri kurekebisha mipangilio ya Kikundi ili kuruhusu kwa muda wasimamizi pekee kutuma ujumbe ikiwa mazungumzo fulani ya Kikundi yameshindwa kudhibitiwa. Hii itakuruhusu kusitisha mazungumzo na kuruhusu washiriki watulie huku ukizingatia hatua zako zinazofuata.
Kutoelewana kidogo kunaweza kuwa mabishano makubwa kwa haraka wakati wanajumuiya wanapohisi kutishwa au kutengwa. Kwa kuwasiliana na wanajumuiya kwa faragha unaonyesha kuwa unajali na uko tayari kusaidia. Inaonyesha kwamba unaelewa nia na maoni yao na huwasaidia kutambua jinsi wanavyoweza kuchangia vyema na kupona kutokana na migogoro. Kumbuka, wakati mwingine watu wanahitaji kutulia kwanza kabla ya kuzungumzia kilichotokea na jinsi wanavyohisi. Wape wanajumuiya muda wa kupumzika na kutulia kabla ya majadiliano zaidi.
Eleza sheria ambazo wanaweza kuwa wamezivunja na usikilize kwa makini ili wahisi wamesikizwa na kuheshimiwa. Jaribu kupata kiini cha tatizo ili uweze kuelewa hisia zao na kwa nini suala hilo lilizuka. Kumbuka kwamba hata watu wakali wanaweza kuhisi kupuuzwa au kutothaminiwa hivyo kuwa wazi na mwenye huruma, hata wakati wa kutekeleza sheria.
Hata hivyo, ikiwa upatanishi haufanyi kazi na wanajumuiya wanaendelea kuwa wakali, fikiria kuwaondoa kwenye Kikundi au jumuiya yako.
Jumuiya yenye afya njema na inayostawi inaruhusu maoni tofauti na mitazamo tofauti. Tumia sheria za jumuiya yako kuwafahamisha wanajumuiya jinsi wanavyotarajiwa kutangamana na wengine. Hili linaweza kuchochea jumuiya yenye heshima, jumuishi inayokubali na kufurahia utofauti.
Ni muhimu kuwa mfano wa tabia unazotaka kuona katika jamii yako. Kwa kuhakikisha kuwa timu yako ya wasimamizi ina wanajumuiya kutoka asili mbalimbali ambao huleta uwezo, mawazo na mbinu tofauti, unaweza kujenga msingi thabiti wa utofauti na ujumuishaji.
Jaribu kukuza heshima katika mikinzano na utafute suluhisho kwa kuhimiza uelewa na heshima kwa washiriki wa asili na maoni tofauti. Wape fursa wanajumuiya kuzungumza kuhusu hali zao na kushiriki hadithi zao. Kufahamu zaidi kuhusu jumuiya yako ni njia nzuri ya kuunda miingiliano na kuwasaidia wanajumuiya kugundua watu wanaoweza kusikizana nao.
Kudhibiti migogoro ni ngumu na kunaweza kuchosha kiakili na kihisia. Ni muhimu kufuatilia afya yako ya akili, na kujilinda dhidi ya ubaya. Hakikisha kuwa umetulia na kufikiri vizuri ili uweze kusaidia kutatua matatizo kwa njia bora zaidi. Ikihitajika, waombe wasimamizi wenzako usaidizi.
Ni vyema kufanya kazi kwa karibu na timu yako ya wasimamizi ili kusaidiana na kushiriki jukumu la kuangalia na kudhibiti migogoro katika jumuiya. Tahadharisha timu yako wakati unashughulika na wanajumuiya wenye changamoto na wagumu na jadili hali hiyo nao ili kusikia maoni mengine, jadili suluhu zinazowezekana na kukubaliana juu ya hatua zinazofaa za kuchukua. Ukihitaji, mwombe msimamizi mwenzako azungumze na wanajumuiya wanaohusika.
Itakufaa pia kuangalia mikakati na tafiti ili kujifunza kutoka kwa wengine ambao wamefanikiwa kusuluhisha migogoro kama hiyo.
Kuweka sheria zilizoandikwa vyema ni hatua ya kwanza muhimu ya kudhibiti jumuiya yako. Fahamu jinsi ya kutekeleza sheria ili kutetea maadili ya jumuiya yako, kuwaweka wanachama salama, na kudumisha ustaarabu.