
“Tuna jumuiya kubwa yenye Vikundi vidogo mbalimbali kuhusu masuala tofauti. Ni muhimu kuwa na wasimamizi ambao wamefunzwa kusimamia vikundi kwa weledi, kwa ufanisi na pia kukuza vikundi kwa urahisi."
- Arun, Pinkishe Foundation
Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Kuwakuza na kuwapa mafunzo wasimamizi hukuwezesha kudhibiti jumuiya yako na kushughulikia masuala kwa ufanisi zaidi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuteua wasimamizi wanaostahiki, kubainisha majukumu yao, kuwawezesha na kusaidiana nao kudhibiti migogoro ambayo huenda ikatokea.
“Tuna jumuiya kubwa yenye Vikundi vidogo mbalimbali kuhusu masuala tofauti. Ni muhimu kuwa na wasimamizi ambao wamefunzwa kusimamia vikundi kwa weledi, kwa ufanisi na pia kukuza vikundi kwa urahisi."
- Arun, Pinkishe Foundation
Kama msimamizi, huenda ukahisi 'unahitajika kila wakati'. Kujibu maswali, kushughulikia maombi, na kusuluhisha migogoro, kunaweza kuchosha sana. Kuna hatua mnazoweza kuchukua kwa pamoja ili kuepuka kulemewa na kuweza kushughulikia changamoto zozote zinazoweza kutokea kadri jumuiya yako inavyozidi kukua. Shirikiana na timu yako kubuni mwongozo na michakato wazi ya kubainisha majukumu na kazi ukizingatia uwezo na udhaifu wa mtu binafsi.
Njia bora ya kuteua wasimamizi wako ni kuchagua miongoni mwa wanajumuiya wanaochangia zaidi au wale unaojua wanakuunga mkono katika masuala na maadili ya jumuiya. Unaweza pia kufanya tangazo kutafuta watu wa kujitolea au kuomba wateuliwa. Tathmini watu waliojitolea na walioteuliwa ukizingatia jinsi wanavyoendeleza dhamira yako, shughuli zao katika Vikundi, na historia yao ya kutangamana na washiriki wengine.
Wazo jingine ni kufikiria juu ya kile ambacho wasimamizi wako wanaweza kufanya usichoweza kufanya. Kuwa na wasimamizi wenye uwezo na ujuzi mbalimbali kutakuwezesha kuimarisha ushirikiano na utendakazi. Wakati uo huo, zingatia wasimamizi wanaowakilisha hali mseto iliyopo katika jumuiya yako. Uwezo wao wa kuwakilisha mitazamo anuai ya wanajumuiya unaweza kusaidia katika kuweka mikakati na kudhibiti changamoto zozote zinazohusiana na maudhui au wanajumuiya.
Ni wazo zuri kuwasiliana na wasimamizi wako na kukubaliana kuhusu namna ya kuwaongeza wapya. Jaribu kuhakikisha kuwa wanaelewana nawe na wasimamizi waliopo. Wasimamizi wengi watasaidia kupunguza majukumu, lakini pia wanaweza kuleta uchangamano. Hakikisha wasimamizi wowote wapya ni watu ambao nyote mnahisi mnaweza kufanya kazi nao.
Wasimamizi wa jumuiya wanaweza kuwaondoa wasimamizi wengine. Pia, unaweza kujiondoa wewe mwenyewe, isipokuwa ukiwa mwanzilishi wa jumuiya. Ikiwa msimamizi anataka kuondoka, ijulishe timu yako na utafute mtu mwingine anayefaa kuchukua nafasi yake.
Unaweza kukutana na hali ambapo mwanajumuiya anakataa kupandishwa cheo na kuwa msimamizi, au msimamizi anajiuzulu kutoka kwa jukumu la msimamizi. Iwapo hilo litatokea, ni muhimu kuheshimu chaguo lake, lakini mfikie ili kuelewa wasiwasi na sababu zao.
Unapoongeza wanajumuiya wapya na wasimamizi kwenye jumuiya yako, ni muhimu kuwasaidia kwa mafunzo, zana na nyenzo. Usisahau kumwelekeza hapa - kwenye Kituo cha Mafunzo cha Jumuiya!
Unaweza kuanzisha kikundi cha wasimamizi pekee ili waweze kuwasiliana, kushauriana na kutoa maoni. Mpe msimamizi aliyepo jukumu la kuwa mshauri au rafiki wa msimamizi mpya ili awe na mtu wa kumwendea ili kupata usaidizi na majibu kwa maswali yoyote. Ni vyema kupanga shughuli za kijamii mara kwa mara ili wasimamizi wapumzike na kuimarisha uhusiano wao.
Hakikisha wasimamizi wanafahamu jinsi unavyowathamini, kwa kuwapongeza na kuwashukuru kwa huduma zao.
Usisahau kuangalia dalili za uchovu. Himiza timu yako kuwasiliana na wasimamizi wengine kwa usaidizi. Pumzika ikiwa inahitajika.
Jumuiya yako inapokua, ni muhimu kushiriki na kusawazisha mzigo wa kazi wa wasimamizi wako. Hakika ni shughuli nzuri kuratibu simu za kawaida za kikundi cha wasimamizi ili kushiriki habari, kujadili masuala, na kusikizana kuhusu majukumu.
Kuelewa uwezo na ujuzi tofauti ulio nao katika timu yako kutakusaidia kugawa majukumu na kukubaliana kuhusu vigezo vya wajibu wa kila msimamizi. Kwa mfano, msimamizi mmoja anaweza kuwa bora katika kudhibiti migogoro kwa hivyo unaweza kufikiria kumfanya ashughulikie hali nyeti.
Usisahau kukubaliana kuhusu saa za kazi kwa kila msimamizi huku ukikumbuka kwamba wanajumuiya wako wanaweza kuhitaji usaidizi wa kila mara. Ni vyema kujadili jinsi unavyotarajia wasimamizi kujibu maswali ya wanajumuiya kwa haraka.
Wakati wa kufanya kazi pamoja kama timu, kila wakati kuna uwezekano kwamba migogoro inaweza kutokea. Ikiwa unahisi kuchanganyikiwa au hasira, jiruhusu kupumzika. Ukiona mshiriki wa timu anafadhaika au kukasirika, wasiliana kwa huruma, na upendekeze apumzike kwa muda.
Sikiliza kwa makini na uulize maswali mengi ili kuelewa vyema kinachosababisha kufadhaika kabla ya kuamua jinsi ya kutatua. Unaweza kutaka kuzingatia majukumu mengine ambayo yanaweza kumfaa zaidi.
Kabla ya kumwondoa msimamizi, fanya mazungumzo naye ili kumfahamisha jinsi matendo yake yanavyoathiri wasimamizi wengine na/au jumuiya. Hii ni fursa ya kutoa maoni na kwake kushughulikia tabia yake.
Ikiwa bado hawezi kufanya kazi pamoja na wengine, mwondoe kwenye timu ya wasimamizi lakini mruhusu abaki katika jumuiya yako. Fikiria kutangaza kuhusu mabadiliko hayo, mtakie heri na uendelee mbele.
Jua jinsi jumuiya mbalimbali zinavyotumia Jumuiya za WhatsApp kuungana, kushiriki maelezo na kufanya kazi kwa madhumuni ya pamoja. Kumbuka kusherehekea mafanikio yao.