Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha jumuiya mpya au unapoongeza vikundi katika Jumuiya kwenye WhatsApp.
Wawezeshe na kushirikiana na wasimamizi na wanajumuiya ili kujenga na kudumisha jumuiya inayowafaa.
Angalia jinsi watu kutoka sekta mbalimbali wanavyotumia WhatsApp kukuza jumuiya zao.
Kuwa sehemu ya jumuiya thabiti hutuwezesha kuwa na uhusiano wa karibu na wengine. Hebu tuangazie umuhimu wa kubainisha madhumuni ya Jumuiya, na jukumu la wasimamizi katika kudumisha mazingira yanayowawezesha wanajumuiya kuheshimiana na kushiriki kwa hiari. Fahamu jinsi ya kuweka sheria madhubuti, na kuteua wasimamizi wanaostahiki ili kukusaidia kudhibiti jumuiya yako kwa ufanisi.
Tutatoa miongozo mingi mahususi, lakini itakuwa kujitolea kwako, shauku na madhumuni yako ambayo yanaleta jumuiya yako pamoja.
"Jumuiya za WhatsApp husaidia kuratibu mada ndogondogo ndani ya kikundi, kuwezesha mchango mzuri wa wanajumuiya na upokeaji wao wa habari."
- Nirveen, Moms in Prenzlauer Berg
Jumuiya ni kikundi cha watu wanaokuja pamoja kwa kuwa mahitaji yao na mambo yanayowavutia ni sawa. Kwenye WhatsApp, kujenga jumuiya ni jitihada - zinazochochewa na malengo yanayoendana na ari, sababu, na hali zilizo muhimu kwa wanajumuiya. Inatoa nafasi ya faragha na salama kwa wanachama kushiriki, kuunganisha, na kugundua vikundi vipya ambavyo wanavutiwa navyo.
Iwe unaunda Jumuiya mpya au unaleta Vikundi vilivyopo pamoja, fikiria kuhusu madhumuni yako, hadhira na jukumu la wasimamizi katika timu yako.
Jumuiya hukuruhusu kupanga mazungumzo kulingana na mada na kudhibiti upakiaji wa habari kupita kiasi kwa kutoa chaguo la kuwasiliana na wanajumuiya wote kwa wakati mmoja - kupitia Kikundi cha Matangazo.
Hebu tuangalie vipengee hivi vinne muhimu vya usimamizi wa Jumuiya:
Kila jumuiya ina madhumuni, sababu ya kuleta watu pamoja inayobainisha chanzo na jinsi wanajumuiya wanavyopaswa kuingiliana. Kwa shule, inaweza kuwa kushiriki ratiba zilizosasishwa, kwa wanaojitolea, kutafuta njia bora ya kuhamasisha, kwa mashabiki wa kandanda, kusaidia timu wanayoipenda katika msimu mzima.
Ni utaratibu mzuri kutambua na kuwasilisha kile unacholenga kuafikia kwa pamoja na manufaa kwa wanajumuiya wako. Kusudi lililo wazi huwasaidia washiriki kuelewa jinsi wanavyoweza kuchangia.
Anza kwa kujiuliza maswali machache rahisi:
Baada ya kubainisha madhumuni, endelea na kuanzisha Jumuiya yako ya WhatsApp. Utahitaji:
Katika kujenga na kukuza desturi nzuri, ni muhimu kuhakikisha kuwa wanajumuiya wamejiunga kwenye jumuiya kwa sababu zinazofaa. Zingatia:
Huu hapa mfano: jumuiya ya shule ina wazazi, walimu, na wanafunzi kutoka madarasa mengi. Baadhi ya matangazo yanawahusu watu hao wote – matangazo kuhusu kurudi shuleni, kufungwa kwa shule, mikutano. Mazungumzo mengine yanahusu tu baadhi ya watu hao – mafunzo ya ualimu, safari ya nyanjani kwa wanafunzi wa darasa la nne, mechi ya soka.
Waza kuhusu hadhira yako na jinsi wanavyoweza kugawanywa katika vikundi vidogo. Hii ni muhimu katika kubaini ikiwa unapaswa kujumuisha pamoja vikundi vilivyopo, au kuanzisha vikundi vipya kwenye jumuiya yako.
Wanajumuiya wapya wanapojiunga, mada mpya na mahusiano yatachipuka kati ya watu. Kama msimamizi wa jumuiya, una uwezo wa kuongeza na kuondoa washiriki na vikundi ili kuhakikisha jumuiya inawafaa waliosalia kadri inavyozidi kukua.
Jinsi ya kumualika mwanajumuiya
Jinsi ya kuwaondoa wanajumuiya
Wasimamizi wa jumuiya wana jukumu muhimu katika kudhibiti na kuhimiza mwingiliano kati ya wanajumuiya, na kudumisha usalama na ujumuishaji kwenye jumuiya. Ili kukuwezesha kutekeleza majukumu yako, Jumuiya kwenye WhatsApp zina zana unazoweza kutumia kudhibiti vikundi na washiriki, na kuhakikisha hali ya utumiaji inayowafaa wanajumuiya.
Kama msimamizi wa jumuiya, una jukumu la kujenga na kudumisha jumuiya. Utafanya hivi kwa kudhibiti mazungumzo huku ukiweka jumuiya yako salama. Ndani ya jumuiya, kila kikundi kina wasimamizi wa kikundi chao, ambao wana jukumu la kusimamia kikundi chao. Kwenye jumuiya inayosimamiwa vyema, wasimamizi wa jumuiya na wa vikundi huwasiliana na wanajumuiya mara kwa mara, na kuwakumbusha kuzingatia sheria za jumuiya.
Katika Jumuiya kwenye WhatsApp, unaweza kuokoa muda kwa kutuma matangazo kwa wanajumuiya wote kupitia kikundi cha Matangazo. Kuleta vikundi chini ya mwavuli wa jumuiya moja huondoa hitaji la kufanya matangazo mengi katika kiwango cha kikundi. Unda na uwasilishe sheria za jumuiya yako mapema ili kuweka matarajio ya utamaduni mzuri tangu mwanzo. Sheria madhubuti hufafanua jinsi wanajumuiya wanaweza kuingiliana kwa njia inayofaa na kuchangia kwenye jumuiya. Sheria zinaweza kusaidia kuzuia migogoro na kuwalinda wanajumuiya.
Zingatia sheria zifuatazo unapounda kanuni za jumuiya yako:
Ni vyema kujumuisha sheria kwenye maelezo ya jumuiya na kuzichapisha katika kikundi cha Matangazo. Wakumbushe wanajumuiya kwamba kutofuata sheria hizi kunaweza kuwapelekea kuondolewa kwenye jumuiya. Pia ni muhimu kushirikiana na wasimamizi wa vikundi ili kuhakikisha sheria za jumuiya zinazingatiwa katika mazungumzo ya vikundi.
Kadri jumuiya yako inavyozidi kukua ndivyo majukumu yako pia yataongezeka. Katika jumuiya kubwa zenye vikundi vingi, huenda ukahitaji timu ya wasimamizi kugawana majukumu. Hii husaidia kuhakikisha kuwa majukumu yanaendelea kudhibitiwa kwa kila mtu anayehusika, na hayategemei mtu mmoja pekee.
Una uwezo wa kugawa hadi majukumu 20 ya wasimamizi wa jumuiya kwa wasimamizi wengine wa kikundi au wanajumuiya. Unapozingatia ni nani wa kupandisha cheo kwa timu yako ya msimamizi, zingatia yafuatayo:
Anzisha kikundi cha Wasimamizi pekee kitakachowashirikisha wasimamizi wa jumuiya na wa vikundi kwa madhumuni ya kuwasiliana na kusaidiana.
Ili kudhibiti kazi na ustawi wa washiriki wa timu yako, ni muhimu kufikiria na kujadili kuhusika kwako tangu mwanzo:
Usalama ni muhimu kwa ustawi wetu. Elewa jinsi masuala ya usalama, faragha na ulinzi yanavyoathiri jumuiya yako na jinsi ya kuwaweka wanajumuiya wako salama na wameunganishwa.